YANGA
SC imengukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika hatua
ya 32 Bora ya Ligi ya Mabingwa kufuatia sare ya 0-0 na wenyeji, Zanacio
katika
mchezo wa marudiano jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Mashujaa,
Lusaka nchini Zambia.
Matokeo
hayo yanamaanisha Yanga inatolewa kwa mabao ya ugenini, baada ya
kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga
wataumia zaidi kwa kutolewa na Zanaco, kwani bao la kusawazisha la
Wazambia hao Dar es Salaam lililopatikana dakika ya 78 kupitia kwa
mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame lilikuwa la kuotea
Na
pamoja na hayo, wachezaji wa Yanga walikuwa wamezubaa kusubiri
wapinzani wao watoe nje mpira kiungwana (Fair Play) baada ya mchezaji
mwenzao, Obrey Chirwa kuangushwa.
Siku
hiyo, Yanbga ilitangulia kwa bao la winga Simon Happygod Msuva dakika
ya 39 baada ya kuwachambua mabeki wa Zanaco kufuatia pasi nzuri ya
kiungo Mzambia, Justin Zulu.
Na
ushindi huu unaifanya Zanaco iendeleze rekodi ya kuitupa nje Yanga
kwenye michuano ya Afrika, baada ya mwaka 2006 pia kuwatoa katika hatua
kama hii ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakishinda 2-0
Lusaka baada ya kufungwa 2-1 Dar es Salaam.
Yanga
sasa itamenyana na timu iliyofuzu hatua ya 32 Bora ya Kombe la
Shirikisho kuwania tikeit ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo,
wakati Zanaci inakwenda moja kwa moja hatua ya makundi ya Ligi ya
Mabingwa.
Kikosi
cha Yanga leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji,
Kevin Yondan, Vincent Bossou, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Haruna
Niyonzima, Simon Msuva, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya/Emmanuel
Martin dk62.
Zanaco;
Toster Sambata, Ziyo Tembo, George Kilufya, Zimeselema Moyo, Chongo
Chirwa, Saith Sakala, Taonga Bwembya, Ernest Mbewe, Boyd Musonda, Attram
Kwame na Augustine Mulenga.
Na Jeff Leah, LUSAKA

0 comments:
Post a Comment