Tuesday, 28 March 2017

TAIFA STARS WAITUMBUA BURUNDI YA KINA MAVUGO, MSUVA, MBARAKA WAKING'ARA



Taifa Stars imeendeleza ushindi baada ya kuitwanga Burundi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars inashinda mechi ya pili mfululizo baada ya kuitwanga Botswana kwa mabao 2-0, Jumamosi iliyopita.

Huku ikicheza bila nahodha wake, Mbwana Samatta ambaye amerejea mapema Ubelgiji kujiandaa na michuano ya Europa League, ilionyesha kiwango kizuri.

Ushindi wa leo haukuwa rahisi kutokana na umahiri wa wachezaji wa Burundi wakiongozwa na Laudit Mavugo.

Stars liana kupata bao lake la kwanza kupitia Simon Msuva ambaye aliunganisha krosi ya Mohamed Zimbwe iliyotua kichwani mwa Ibrahim Ajibu kabla ya kumfikia mchungaji.

Mavugo aliisawazishia Burundi akimhadaa Deogratius Munishi aliyetoka langoni mapema.

Lakini Mbaraka Yusuf anayetokea Kagera Sugar, ikiwa ndiyo anaanza kuichezea Stars, akafunga bao zuri kabisa baada ya mpira wake wa kwanza kugonga mwamba, lakini akamalizia kwa shuti la mguu wa kushoto.


Juhudi za Burundi kukomboa au Taifa Stars kuongeza, hazikuzaa matunda hadi mwisho wa dakika 90.
Credit: Salehe jembe

RATIBA YA ASFC YAPANGWA - YANGA KUMENYANA NA PRISONS APRILI 22, 2017


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini limetoa ratiba ya michezo miwili ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federations Cup (ASFC) kwa timu za Yanga na Azam ambazo zilikuwa hazijapangwa.Mechi hizo zilishindikana kuchezwa baada ya Yanga na Azam kuwa wawakilisji katika michuano ya kimataifa ambapo April 95 Azam itashuka dimbani kuvaana na Ndanda kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.Yanga ambao bado wanaendelea kuiwakilisha nchi kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika wao mchezo wao utakuwa April 22 watakapovaana na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa.Taarifa kutoka TFF zimesema kwamba michezo miwili ya mwisho ya Robo Fainali za ASFC zimepangiwa tarehe na pazia la nane bora litafungwa Aprili 22.Tayari Simba ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza zimekwishafuzu hatua ya Nusu Fainali baada ya kuzitoa Kagera Sugar ya Bukoba na Madini FC ya Arusha katika Robo Fainali.Mbao FC iliwafunga Kagera Sugar 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Simba SC iliwafunga Madini FC 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha bao pekee la Mrundi, Laudit Mavugo.Kikosi cha Prisons FCKikosi cha Yanga
Michuzi

Wednesday, 22 March 2017

YANGA YAWAONDOA HOFU MASHABIKI, WASEMA MC ALGER NI KAMA TIMU NYINGINE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wanashukuru wamepata ratiba kwa wakati ya hatua ya mtoano wa kombe la Shirikisho na mechi ya kwanza wanaanzia hapa nyumbani dhidi ya wapinzani wao MC Alger toka Algeria.
Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kuwa hawana hofu na MC Alger kwani ni kama timu nyingine na kikubwa zaidi amewaondoa hofu mashabiki na kuwataka watulie kwani benchi la ufundi linaendelea kukinoa kikosi kwa ajili ya maandalizi.
" Yanga SC ni timu kongwe na bora na tumejipanga kupata matokeo nyumbani na ugenini. Tumezungumza na wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi kujiandaa vyema kimbinu , kiufundi na kisaikolojia kushinda mchezo huu. Mechi kama hizi unapopata ushindi mzuri wa nyumbani , basi unapunguza mlima wa kuupanda ugenini,"amesema Mkwasa.
Mkwasa amesema kuwa MC Alger ni timu nzuri na amekuwa bingwa wa Afrika hivyo kila mtu atataka kuiona na sisi tunawaheshimu kwa historia yao lakini tunakwenda kupambana kutafuta ushindi na zaidi ameweka wazi msisitizo kuwa hivi karibuni wame
"muda ukifika tutawajuza wapi mechi itafanyikia kama ni hapa jijini au popote Tanzania. Kwa sasa bado hatujaamua lolote katika hilo hivyo uwanja wa taifa unabaki kutambulika kama uwanja wa nyumbani."
Mkwasa akizungumzia sapoti ya mashabiki katika mchezo wao , alieleza kinagaubaga jinsi gani klabu inahitaji sapoti yao mwanzo mwisho , " mashabiki na wadau wote wa soka nchini tunawaomba kuipa sapoti timu yetu muda wote wa dakika 90 itakapokuwa uwanjani.
"tunawafahamu vyema wenzetu kwa fitina zao hususani mechi za kwao . Mara nyingi huzipanga usiku ili wapate fursa ya kuwasha miale yao na vitochi kuumiza macho ya wachezaji . Tunawaandaa wachezaji wetu katika hali zote pia umakini wa kuripoti kila tukio kwa mamlaka husika . " alimaliza katibu mkuu huyo wa Yanga SC ndugu Charles Mkwasa.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa

Monday, 20 March 2017

YANGA YAANGUKIA KOMBE LA SHIRIKISHO, ZANACO YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA

YANGA SC imengukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika hatua ya 32 Bora ya Ligi ya Mabingwa kufuatia sare ya 0-0 na wenyeji, Zanacio katika 
mchezo wa marudiano jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia.
Matokeo hayo yanamaanisha Yanga inatolewa kwa mabao ya ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Yanga wataumia zaidi kwa kutolewa na Zanaco, kwani bao la kusawazisha la Wazambia hao Dar es Salaam lililopatikana dakika ya 78  kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame lilikuwa la kuotea
Na pamoja na hayo, wachezaji wa Yanga walikuwa wamezubaa kusubiri wapinzani wao watoe nje mpira kiungwana (Fair Play) baada ya mchezaji mwenzao, Obrey Chirwa kuangushwa.
Siku hiyo, Yanbga ilitangulia kwa bao la winga Simon Happygod Msuva dakika ya 39 baada ya kuwachambua mabeki wa Zanaco kufuatia pasi nzuri ya kiungo Mzambia, Justin Zulu.
Na ushindi huu unaifanya Zanaco iendeleze rekodi ya kuitupa nje Yanga kwenye michuano ya Afrika, baada ya mwaka 2006 pia kuwatoa katika hatua kama hii ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakishinda 2-0 Lusaka baada ya kufungwa 2-1 Dar es Salaam. 
Yanga sasa itamenyana na timu iliyofuzu hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho kuwania tikeit ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, wakati Zanaci inakwenda moja kwa moja hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya/Emmanuel Martin dk62.
Zanaco; Toster Sambata, Ziyo Tembo, George Kilufya, Zimeselema Moyo, Chongo Chirwa, Saith Sakala, Taonga Bwembya, Ernest Mbewe, Boyd Musonda, Attram Kwame na Augustine Mulenga.

 Na Jeff Leah, LUSAKA

Thursday, 16 March 2017

Hili ndio jeshi kamili liliondoka kwenda kuikabili Zanaco ya Zambia kwenye mechi ya marudiano Klabu Bingwa Afrika





Klabu ya soka ya Yanga SC inapenda kutoa taarifa juu ya safari yake kuelekea Zambia katika mechi ya marudiano dhidi ya Zanaco FC.
Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi unaondoka jioni hii saa 11:15 kwa ndege ya shirika la Kenya Airways.
Wachezaji wanaondoka ni Makipa; Deogratius Munishi na Ali Mustafa . Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.
Nafasi ya viungo ni; Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima,Saidi Makapu, Deusi Kaseke, Juma Saidi, Justine Zulu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva na Geofrey Mwashuiya. Upande wa washambuliaji ni Obrey Chirwa na Emanuel Martin.
Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali zikiwemo majeruhi ; Malimi Busungu,Beno Kakolanya, Mateo Antony , Pato Ngonyani , Amisi Tambwe , Yusufu Mhilu na Donald Ngoma.
Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano; Young Africans SC
15.03.2017

Yanga kumkosa Donald Ngoma kwa msimu mzima uliobakia

Klabu ya Yanga atakosa huduma ya mshambuliaji wake Mzimbabwe, Donald Ngoma, baada ya mchezaji huyo kurudishwa hospitali kwa ajili ya kuendelea na matibabu ya goti ambayo yanamsumbua kwa muda mrefu
Daktari wa timu ya Yanga Edward Bavu, ameuambia mtandao wa Goal, Ngoma hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kujitonesha goti hilo Jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Zanaco.
“Nimemshauri kocha kumuondoa kwenye orodha ya wachezaji watakao kwenda Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano kwasababu hali yake siyo nzuri na nimelazimika kumuanzishia matibabu upya,”amesema Bavu.
Daktari huyo amesema kwa namna alivyogundua ukubwa wa tatizo hilo, anafikiria mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima uliobakia na anaweza kuwa tayari hadi mwanzoni mwa msimu ujao wa ligi ya Vodacom.
Amesema awali walidhani tatizo hilo litakuwa dogo lakini baada ya kuliangalia kwa undani wamebaini kuwa ni tatizo kubwa ambalo linahitaji kupata tiba maalumu ili aweze kupona na kurejea kwenye majukumu yake ya kuipigania Yanga.
Ngoma kabla ya taarifa hizo alirejea uwanjani katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Jumamosi lakini hakuweza kumaliza mchezo na kutolewa kipindi cha pili.
Kikosi cha Yanga kinaondoka Alhamisi kuelekea Zambia kwa ajili ya pambano hilo la marudiano na Zanaco na hadi sasa hakuna matumaini ya nyota huyo muhimu kutoka Zambia kuwa anaweza kutoa mchango wake.
Source: Goal

Monday, 13 March 2017

MAJINA 26 YA WACHEZAJI WALIOITWA NA KOCHA MAYANGA TAIFA STARS

March 13 2017, kocha wa muda wa timu ya Taifa la Tanzania Salum Mayanga alitangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Taifa Stars. Mayanga ambaye amerithi nafasi hiyo kutoka kwa kocha Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya wachezaji hao leo.
Wachezaji hao wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA.
Goalkeepers                 
-Deo Munishi
-Aishi Manula
-Said Mohamed
Defenders
-Erasto Nyoni
-David Mwantika
-Hassan Kessy
-Mohamed Hussein
-Salim Mbonde
-Abdi Banda
-Shomari Kapombe
-Gadiel Michael
Midfielders
-Himid Mao
-Jonas Mkude
-Said Ndemla
-Mzamiru Yassin
-Salum Abubakari
-Frank Domayo
Wingers
-Simon Msuva
-Farid Mussa
 -Shiza kichuya
-Hassan Kabunda
Forwads
-Mbaraka Yusuph 
-Abdulrahman Mussa
-Ibrahim Hajibu
-Thomas Ulimwengu
-Mbwana Samatta